1. Kuhusu masharti haya
Masharti haya yanaongoza matumizi ya Shule Masta — mfumo wa kusimamia shule, tovuti za shule, fomu za udahili mtandaoni na app ya wazazi — inayoendeshwa na Pamui Afrika, Dar es Salaam, Tanzania ("sisi"). Kwa kutumia huduma, unakubali masharti haya. Kama shule ina mkataba maalum na sisi, masharti ya mkataba huo yanatangulia pale yanapotofautiana na haya.
2. Huduma
Tunaipa shule mfumo wa mtandaoni wa kusimamia wanafunzi, ada na fedha, mitihani na ripoti, mahudhurio, udahili, tovuti ya shule na mawasiliano na wazazi, pamoja na app ya wazazi. Tunaweza kuboresha au kubadilisha sehemu za huduma; hatutaondoa kipengele kikuu ambacho shule inalipia bila kuipa taarifa mapema.
3. Akaunti
- Shule inawajibika kwa watumishi inaowapa akaunti na ruhusa wanazopewa.
- Kila mtumiaji atunze nenosiri lake kwa siri na asishirikiane akaunti na mtu mwingine.
- Mkiona matumizi yasiyoruhusiwa, tujulisheni mara moja.
4. Ada na malipo
- Bei ni TSh 6,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ikijumuisha moduli zote, tovuti ya shule, udahili mtandaoni na app ya wazazi.
- Shule inaweza kulipa kila robo mwaka (TSh 1,500 kwa mwanafunzi), kila nusu mwaka (TSh 3,000 kwa mwanafunzi) au mwaka mzima kwa punguzo la 10% (TSh 5,400 kwa mwanafunzi).
- Ankara inatolewa mwanzoni mwa kila kipindi kulingana na idadi ya wanafunzi wanaoendelea na masomo, na inalipwa ndani ya muda ulioandikwa kwenye ankara.
- Malipo yasipofanyika kwa wakati, tutaikumbusha shule kwanza; malipo yakichelewa zaidi tunaweza kusimamisha huduma kwa muda baada ya kutoa taarifa. Taarifa za shule hazifutwi kwa sababu ya kuchelewa kulipa.
- Tukibadilisha bei, tutaijulisha shule angalau siku 30 kabla; bei mpya itaanza kipindi kinachofuata cha malipo.
5. SMS na mawasiliano
Kutuma ujumbe kumo ndani ya huduma, lakini SMS zinalipiwa kando kwa TSh 20 kwa kila SMS kutoka salio la SMS la shule. Shule inawajibika kwa maudhui ya ujumbe inaotuma, na inapaswa kutuma ujumbe unaohusu shule tu kwa wazazi waliosajiliwa nayo. Taarifa za app (push) kwa wazazi wanaotumia app hazilipiwi.
6. Taarifa za shule
- Taarifa ambazo shule inaingiza ni mali ya shule. Tunazitumia tu kutoa huduma kwa shule, kama ilivyoelezwa kwenye Sera ya Faragha.
- Shule inawajibika kuwa na haki ya kukusanya na kuingiza taarifa hizo, na kuwajulisha wazazi na watumishi kuhusu matumizi yake.
- Shule ikiomba, tunaipa nakala ya taarifa zake.
7. Matumizi yanayokubalika
Usitumie huduma:
- kwa jambo lolote lisilo halali, au kutuma ujumbe wa udanganyifu, matangazo yasiyoombwa au maudhui ya kuudhi;
- kujaribu kuingia kwenye akaunti au taarifa za shule nyingine;
- kuvuruga, kushambulia au kujaribu kuvunja usalama wa mfumo;
- kunakili, kuuza au kutengeneza upya mfumo wenyewe.
8. Wazazi
App ya wazazi ni bure. Mzazi anaona taarifa za watoto wake tu, kama zilivyowekwa na shule. Maswali kuhusu alama, ada au taarifa za mwanafunzi yaelekezwe kwa shule kwanza. Mzazi anaweza kufuta akaunti yake ya app wakati wowote kupitia Futa akaunti.
9. Upatikanaji
Tunajitahidi huduma ipatikane muda wote, lakini kunaweza kuwa na vipindi vya matengenezo au hitilafu zisizotarajiwa. Matengenezo yaliyopangwa tutayafanya kwa kadiri inavyowezekana nje ya saa za shule.
10. Kusitisha huduma
- Shule inaweza kuacha kutumia huduma mwisho wa kipindi chochote cha malipo kwa kutujulisha kwa maandishi.
- Tunaweza kusitisha huduma kama masharti haya yamevunjwa kwa kiasi kikubwa na hayajarekebishwa baada ya taarifa.
- Baada ya kusitisha, tunaipa shule nakala ya taarifa zake ikiomba, kisha tunazifuta ndani ya siku 90.
11. Dhima
Tunatoa huduma kwa uangalifu na weledi. Kwa kadiri sheria inavyoruhusu, hatuwajibiki kwa hasara isiyo ya moja kwa moja, na jumla ya dhima yetu kwa shule kwa madai yoyote haitazidi kiasi ambacho shule ilitulipa katika miezi 12 iliyotangulia madai hayo. Hakuna kipengele katika masharti haya kinachoondoa dhima ambayo sheria hairuhusu kuiondoa.
12. Sheria inayotumika
Masharti haya yanaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tutajaribu kwanza kumaliza tofauti yoyote kwa mazungumzo; isipowezekana, itapelekwa kwenye mahakama za Tanzania.
13. Mawasiliano
Pamui Afrika — Shule Masta
Dar es Salaam, Tanzania
Barua pepe: [email protected]
WhatsApp: 0753 276 939
1. About these terms
These terms govern the use of Shule Masta — the school management system, school websites, online admission forms and the parent app — operated by Pamui Afrika, Dar es Salaam, Tanzania ("we", "us"). By using the service you agree to these terms. Where a school has a separate written agreement with us, that agreement takes precedence where it differs.
2. The service
We provide schools with an online system for students, fees and finance, exams and report cards, attendance, admissions, the school website and communication with parents, plus the parent app. We may improve or change parts of the service; we will not remove a core feature a school pays for without notice.
3. Accounts
- The school is responsible for the staff it gives accounts to and the permissions they receive.
- Every user must keep their password secret and must not share their account.
- Tell us straight away if you notice unauthorised use.
4. Fees and payment
- The price is TSh 6,000 per student per year, including all modules, the school website, online admissions and the parent app.
- Schools may pay every quarter (TSh 1,500 per student), every half-year (TSh 3,000 per student) or for the whole year with a 10% discount (TSh 5,400 per student).
- An invoice is issued at the start of each period based on the number of active students, and is due within the time stated on the invoice.
- If payment is late we will remind the school first; if it remains unpaid we may suspend the service after notice. A school's data is never deleted because of late payment.
- If we change the price, we will give at least 30 days' notice; the new price applies from the next billing period.
5. SMS and messaging
Messaging is part of the service, but SMS are charged separately at TSh 20 per SMS from the school's own SMS balance. The school is responsible for the content it sends and should only send school-related messages to parents registered with it. App (push) notifications to parents who use the app are free.
6. Your school's data
- Information a school enters belongs to the school. We use it only to provide the service, as described in our Privacy Policy.
- The school is responsible for having the right to collect and enter that information, and for informing parents and staff about its use.
- On request, we give the school a copy of its information.
7. Acceptable use
You must not use the service:
- for anything unlawful, or to send fraudulent, unsolicited promotional or offensive messages;
- to try to access another school's accounts or information;
- to disrupt, attack or try to break the security of the system;
- to copy, resell or rebuild the system itself.
8. Parents
The parent app is free. Parents see only their own children's information, as entered by the school. Questions about marks, fees or student records should go to the school first. Parents can delete their app account at any time via Delete account.
9. Availability
We aim to keep the service available at all times, but there may be maintenance windows or unexpected outages. Planned maintenance is done outside school hours wherever possible.
10. Ending the service
- A school may stop using the service at the end of any billing period by telling us in writing.
- We may end the service if these terms are seriously breached and not put right after notice.
- After the service ends, we give the school a copy of its information on request, then delete it within 90 days.
11. Liability
We provide the service with reasonable care and skill. As far as the law allows, we are not liable for indirect loss, and our total liability to a school for any claim will not exceed the amount the school paid us in the 12 months before the claim. Nothing in these terms excludes liability that cannot be excluded by law.
12. Governing law
These terms are governed by the laws of the United Republic of Tanzania. We will first try to settle any disagreement by discussion; if that fails, it will go to the courts of Tanzania.
13. Contact
Pamui Afrika — Shule Masta
Dar es Salaam, Tanzania
Email: [email protected]
WhatsApp: 0753 276 939